PROSHABO ONLINE SCHOOLS KISWAHILI MTAALA – KISWAHILI: KIDATO CHA 1

MTAALA – KISWAHILI: KIDATO CHA 1

Categories:

Mada ya 1: Mawasiliano
a). Lugha kama Chombo cha Mawasiliano
i. Elezea maana ya mawasiliano
ii. Fafanua dhima za lugha katika mawasiliano
iii. Fafanua matumizi na umuhimu wa lugha

b). Matamshi na Lafudhi ya Kiswahili
i. Elezea maana ya matamshi
ii. Bainisha sauti za lugha ya Kiswahili
iii. Elezea kuhusu lafudhi ya Kiswahili

Mada ya 2: Aina Za Maneno
a). Ubainishaji wa aina Saba za Maneno
i. Bainisha aina saba za maneno ya Kiswahili

b). Ufafanuzi wa aina za Maneno
i. Elezea maana ya kila aina ya neno

c). Matumizi ya aina za Maneno katika Tungo
i. Elezea matumizi ya aina za maneno katika tungo

d). Matumizi ya Kamusi
i. Elezea maana ya Kamusi
ii. Elezea jinsi ya kutumia kamusi
iii. Fafanua taarifa ziingizwazo katika kamusi

Mada ya 3: Fasihi Kwa Ujumla
a). Dhima ya Fasihi
i. Elezea dhana ya fasihi
ii. Fafanua dhima za fasihi katika jamii

b). Aina za Fasihi
i. Fafanua dhana ya fasihi simulizi
ii. Elezea sifa na dhima za fasihi simulizi
iii. Fafanua dhana ya fasihi andishi
iv. Elezea sifa na dhima za fasihi andishi
v. Onesha tofauti kati ya fasihi andishi na fasihi simulizi

Mada ya 4: Fasihi Simulizi
a). Ubainishaji wa Tanzu za Fasihi Simulizi
i. Bainisha tanzu za fasihi simulizi

b). Ufafanuzi wa Vipera vya Tanzu za Fasihi Simulizi
i. Fafanua vipera vya hadithi
ii. Fafanua vipera vya ushairi
iii. Fafanua vipera vya semi
iv. Fafanua vipera vya maigizo

c). Uhakiki wa kazi za Fasihi Simulizi
i. Elezea umuhimu wa uhakiki wa kazi za fasihi simulizi
ii. Elezea vigezo vya uhakiki wa kazi za fasihi simulizi
iii. Elezea uhakiki wa hadithi
iv. Hakiki matumizi ya semi katika hadithi

Mada ya 5: Usimulizi
a). Usimulizi wa Hadithi
i. Elezea njia za usimulizi wa hadithi

b). Usimulizi wa Habari
i. Fafanua taratibu za usimulizi wa matukio

Mada ya 6: Uandishi Wa Insha
a). Insha za Wasifu
i. Elezea hatua za uandishi wa insha
ii. Fafanua muundo wa insha
iii. Tofautisha insha za kisanaa na zisizo za kisanaa

Mada ya 7: Uandishi Wa Barua
a). Barua za Kirafiki
i. Elezea muundo wa barua za kirafiki

Mada ya 8: Ufahamu
a). Kusikiliza
i. Elezea mambo ya kuzingatia katika ufahamu wa kusikiliza
ii. Jibu maswali kutokana na habari uliyosikiliza

b). Kusoma kwa Sauti
i. Elezea mambo ya Kuzingatia katika ufahamu wa kusoma kwa sauti
ii. Jibu maswali kutokana na habari uliyosoma

c). Kusoma Kimya
i. Jibu maswali kutokana na habari uliyosoma

d). Kusoma kwa Burudani
i. Fafanua mambo ya kuzingatiwa katika ufahamu wa kusoma kwa burudani

Leave a Reply